Mountain biodiversity and the SDGs

Baioanuwai za milimani na malengo endelevu ya kimaendeleo (SDGs)

Background, malengo, na mbinu

Background

Sehemu za milima, idadi ya watu, utofauti wa kibaiolojia na kiutamaduni, na vitu muhimu na huduma zitokanazo na mifumo ikolojia, milima ni ya umuhimu mkubwa wa kiikolojia, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii. Ingawa, mchanganyiko wa shinikizo la kuongezeka kwa idadi ya watu duniani na shinikizo la kiuchumi na umuhimu wa viumbe hai mbalimbali pamoja na thamani itokanayo na huduma za kimazingira (mifumo ikolojia) vinahatarisha ustawi wa milima. Kwa hiyo, maendeleo endelevu ya kiikolojia ya kiuchumi na kijamii katika milima imekuwa na umuhimu na malengo endelevu ya kimaendeleo (SDGs) yamepitishwa kama chombo muhimu cha kuongoza mchakato huu.
Mradi huu unachangia kuelewa vizuri zaidi changamoto zinazohusiana na udhibiti endelevu na uhifadhi wa baioanuwai za milimani (SDG 15.4) katika mazingira ya ushindani kati ya malengo endelevu ya kimaendeleo, rasilimali chache, na miundo tata ya kiutawala.

Malengo

  • Kutathmini hali na mwenendo wa ustawi wa binadamu, viumbe hai, mazingira na huduma za mifumoikolojia katika milima katika ngazi ya kimataifa, ya kitaifa na ngazi za chini za kitaifa kwa kutumia mfumo wa tathmini ya Jukwaa la Sera za Sayansi juu ya baioanuwai na Huduma za mifumoikolojia (Intergovernmental Science-Policy Platform on Biodiversity and Ecosystem Services-IPBES)
  • Kujifunza umuhimu na ushirikiano kati ya baioanuwai zinazohusiana na malengo endelevu ya kimaendeleo (SDG) na malengo mengine endelevu ya kimaendeleo katika milima katika ngazi ya kimataifa, ya kitaifa, na ya kikanda, na kutambua ushirikiano na umuhimu.
  • Kutambua jukumu la muktadha unaotolewa na sababu za kiutawala, uchumi, kiteknolojia, mifumo ya kijamii na kiikolojia, kiutamaduni, kimazingira ambazo huunda ushirikiano huu.
  • Kutoa ujuzi uliopatikana kwa makundi muhimu ya wadau na kuwezesha tathmini ya msingi ya fursa za kutekeleza hatua za kuzingatia kufikia maendeleo ya endelevu ya mazingira, kijamii na kiuchumi.

Mbinu

Somo la kubuni: mradi utafuata njia ya kubuni iliyopangwa katika maeneo yaliyogawanywa na data zilizokusanywa, kuchambuliwa, na kulinganishwa katika ngazi za kimataifa, kitaifa (Bolivia, Nepal, Tanzania), na ngazi za chini za kitaifa. Maeneo ya utafiti katika ngazi ya chini ya nchi itajumuisha kiwango cha muinuko, kutoka chini ya mlima hadi kwenye kiwango cha juu watu wanakoishi, na kiwango cha matumizi ya ardhi, kutoka kwa mazingira asili / yanayohifadhiwampaka maeneo yanayokutumika sana. Ngazi hizi zitatumika kuelewa athari za mambo maalum ya muktadha juu ya uhusiano kati ya mazingira asili na watu, na kwa maoni ya jamii na tafsiri ya vipaumbele vya maendeleo endelevu.

Ukusanyaji wa data: ukusanyaji wa data utahusisha uchanganuzi wa takwimu za wazi na takwimu, tafiti za mtandaoni, ukaguzi wa fasihi unaozingatia vipengele vya mfumo wa IPBES pamoja na taarifa zinazohusiana na SDG; na mahojiano